Kai Flow · Mfumo wa duka

Ujue kilichotokea dukani leo — hata ukiwa mbali.

Wafanyakazi wako wanauza kwenye simu zao. Wewe unaona mauzo, stoo na madeni papo hapo, popote ulipo. Na mtandao ukikatika, mauzo hayasimami.

  • Inafanya kazi kwenye simu ya kawaida
  • Kiswahili kwanza, Kiingereza ukitaka
  • Hakuna mashine mpya ya kununua

Jaribu hapa: uza kitu, kisha zima mtandao uendelee kuuza.

Bidhaa, bei na majina ni ya mfano. Hakuna kinachotumwa popote.

Stoo

Stoo haidanganyi.

Kila kipande kinachotoka au kurudi kinaandikwa pamoja na sababu yake. Uza, rudisha, futa oda — hesabu ya mfumo inabaki sawa na kilicho kwenye rafu. Jaribu kuivuruga.

Ukiwa mbali

Simu yako ndiyo ofisi yako.

Kila oda inakufikia ikishatumwa kutoka dukani. Duka likikatika mtandao, unaambiwa kwamba kuna taarifa zinazosubiri — hupewi namba pungufu inayojifanya kamili.

  • Mauzo, oda na madeni ya leo kwa mtazamo mmoja
  • Unaambiwa bidhaa inapokaribia kuisha
  • Unaamua nani anaona nini — muuzaji hahitaji kuona faida

Kwa kila biashara

Duka lako linauza nini?

Mfumo ni mmoja, lakini unajua tofauti ya kuuza sukari na kuuza friji. Gusa biashara yako — mfano wa juu utabadilika.

Dukani na mtandaoni

Duka moja. Milango mitatu.

Bidhaa zile zile, bei zile zile na stoo ile ile — kaunta, duka lako la mtandaoni na WhatsApp. Oda kutoka popote inaingia mahali pamoja.

  • Kaunta Kai POS kwenye simu ya muuzaji, na risiti kama unaitaka.
  • Duka la mtandaoni Tovuti ya duka lako, kwa jina lako na rangi zako, inayosoma stoo yako halisi.
  • WhatsApp Msaidizi anajibu wateja kuhusu bidhaa na bei hata saa nane usiku, kutoka kwenye orodha yako ya bidhaa.

Kuanza

Hatua tatu, na hatuziachi kwako peke yako.

  1. Tunaongea kuhusu duka lako Unauza nini, una wafanyakazi wangapi, una maduka mangapi. Tunakuonyesha Kai Flow ikiwa na bidhaa za aina yako.
  2. Tunaingiza bidhaa zako Tupe Excel au faili kutoka mfumo wako wa zamani. Tunaingiza bidhaa, bei na stoo kwa niaba yako.
  3. Wafanyakazi wanaanza kuuza Kwenye simu zao, kupitia kiungo. Hakuna app store, hakuna mashine mpya.

Maswali

Maswali tunayoulizwa mara nyingi.

Nahitaji kompyuta au mashine ya POS?

Hapana. Kai Flow inafanya kazi kwenye simu ya kawaida ya Android au iPhone, na kwenye kompyuta ukipenda. Printa ya risiti na skana ya barcode ni hiari.

Mtandao ukikatika inakuwaje?

Mauzo yanaendelea kurekodiwa kwenye simu ya muuzaji, na yanatumwa yenyewe mtandao ukirudi. Kwenye simu yako unaona kwamba kuna taarifa zinazosubiri.

Nina mfumo mwingine tayari. Bidhaa zangu zitahamaje?

Tupe Excel au faili kutoka mfumo wako wa zamani. Tunaingiza bidhaa, bei na stoo kwa ajili yako, na hakuna kinachofutwa ukipakia faili mara ya pili.

Wafanyakazi wataona kila kitu?

Hapana. Kila mfanyakazi anapewa nafasi yake: muuzaji anauza, msimamizi wa stoo anapokea mzigo, na wewe unaamua nani anaona nini.

Gharama ni kiasi gani?

Inategemea ukubwa wa duka na idadi ya maduka. Ongea nasi tukupe bei inayolingana na biashara yako.

Tuonyeshe duka lako. Tutakuonyesha Kai Flow ndani yake.

Ongea nasi WhatsApp